Askari
jeshi wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa kundi haramu Boko Haram wameteka
watu zaidi ya 60 katika nchi jirani ya Cameroon imethibitika.
Inasemekana
miongoni mwa mateka wengi wao ni watoto waliokamtwa mpakani mwa nchi
mbili hizo.Na inaarifiwa kuwa watu kadhaa waliuawa wakati wa utekelezaji
wa tukio hilo.
Boko Haram siku za hivi karibuni zimekamata
udhibiti wa miji kadhaa na vijiji upande wa kaskazini Mashariki mwa
Nigeria, na sasa wameanza kuwa tishio kwa nchi jirani wanazopakana na
Nigeria .Katika shambulio hilo la siku ya Jumapili askari hao walivamia
vijiji viwili vilivyoko eneo la Tourou .
Katika uvamizi huo nyumba
kadhaa zilichomwa moto na idadi ya mateka ni themanini kati yao watu
wazima ni thelathini,na watoto wapatao hamsini na walielekea upande wa
Kaskazini mwa Cameroon .
Kundi hilo limepigana vita takribani miaka sita sasa, wakijaribu kuusimika utawala wa dola ya kiislam nchini humo.
0 comments:
Post a Comment