Katika mwendelezo wa chuki dhidi ya dini na matukufu ya Kiislamu,
Marekani imepiga marufuku adhana katika Chuo Kikuu cha Duke nchini
humo. Chuo Kikuu cha Duke ambacho hivi karibuni kilikuwa kimetoa ruhusa
kwa Waislamu wa chuo hicho kuadhini, kimepiga tena marufuku suala hilo.
Wiki iliyopita, viongozi wa chuo hicho kilichopo katika jimbo la
Carolina kaskazini walitoa taarifa rasmi iliyoruhusu adhana kupitia
mnara wa kanisa shuleni hapo. Awali Michael Schoenfeld, Naibu Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Duke alinukuliwa akisema kuwa, wanafunzi wa Kiislamu
wamekuwa na mchango mkubwa katika ustawi wa chuo na kwamba bodi ya shule
inakubali watekeleze ibada zao shuleni hapo. Hata hivyo ghafla viongozi
wa chuo hicho wamepiga marufuku adhana bila kutolewa sababu maalumu.
Baadhi wanamtaja Franklin Graham, kasisi wa Kimarekani kuwa chanzo cha
marufuku hiyo, hasa kwa kuzingatia kuwa hivi karibuni alitishia kukata
misaada yake kwa chuo hicho ikiwa Waislamu wataruhusiwa kuadhini chuoni
hapo.
0 comments:
Post a Comment