IMEELEZWA kuwa pamoja na
kijiuzulu kwa Profesa Sospeter Muhongo, bado hatua hiyo haitoshi
kutatua tatizo la wizi mzito wa fedha za umma kwakuwa wahusika wakuu wa
uchotaji wa fedha hizo, bado hawajakamatwa na hata kuhojiwa na hivyo
mjadala wa Escrow bado ungali mbichi.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na
Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa CHADEMA Arcado Ntagazwa kwenye
mkutano na waandishi wa habari uliojadili namna sakata la Tegeta Escrow
linavyoendeshwa.
Akifafanua hayo Ntagazwa amesema kuwa hatua madhubuti za
kushughulikia ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya
Tegeta Escrow hazijakamilika na haziwezi kukamilika bila kuhojiwa au
kuwajibishwa kwa Gavana wa benki kuu, Waziri wa fedha na katibu wake
pamoja na maofisa wa Ikulu na Rais mwenyewe ambaye ndiye aliyeruhusu
fedha hizo kutolewa.
0 comments:
Post a Comment