KITUO cha sheria na haki
za binadamu kimelaani vikali kitendo cha kupigwa kwa Mwenyekiti wa
chama cha Wananchi –CUF, Profesa IBRAHIM LIPUMBA na kusema kuwa kitendo
hicho ni cha kinyama.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar e s salaam Mkurugenzi
wa Kituo hicho, HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa kumekuwa na ubaguzi
mkubwa hasa katika vyama vya siasa jambo linalopelekea kuvigawa vyama
hivyo na kuvikosesha haki yao ya msingi.
Aidha amesema kuwa kitendo cha jeshi la polisi kujichukulia sheria
mkononi kwa kumpiga kiongozi huyo na waandishi wa habari ni kitendo cha
kulaaniwa hivyo amelitaka jeshi la polisi kuchukukuliwa hatua za
kinidhamu ili kuweza kukomesha tabia hizo.
0 comments:
Post a Comment