Harakati ya Answarullah ya nchini Yemen, imelaani vikali Baraza
la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi dhidi yake. Ripoti iliyotolewa na
Dhaifullah al-Shami, mjumbe wa baraza la kisiasa la harakati hiyo nchini
Yemen, mbali na kulaani taarifa ya Baraza hilo la Ghuba ya Uajemi
iliyoyataja mabadiliko ya Sana'a kuwa ni mapinduzi ya kijeshi, imesema
kuwa matukio yanayojiri nchini Yemen yanatokana na uingiliaji wa baraza
hilo na Saudia. Dhaifullah amesema kuwa hotuba ya Abdul-Malik al-Huthi,
kiongozi wa harakati hiyo zimewafanya viongozi wa baraza hilo kupatwa na
kiwewe na hivyo kuibua propaganda kupitia vyombo vyao vya habari dhidi
ya harakati hiyo. Amesema kuwa, tangu asubuhi ya Alkhamis iliyopita
Harakati ya Answarullah ilianza kutekeleza ahadi yake kwa mujibu wa
makubaliano mapya nchini humo. Ameongeza kuwa, matukio ya hivi karibuni
nchini Yemen yalikuwa yanaandaa utekelezwaji wa njama za Saudia na
baraza hilo la Ghuba ya Uajemi kwa lengo la kuizingira harakati hiyo na
kuibua vita vya ndani nchini humo njama ambazo hata hivyo zimefeli.
0 comments:
Post a Comment