Ni
miaka 26 tangu tuone viatu vikijifunga kamba zenyewe kama ilivyokuwa
kwenye matangazo ya biashara ya viatu vya Nike vyake Marty McFly
vikijifunga miaka hio. hio
Hilo lilikuwa tu tangazo la bishara
zamani sana lakini kuna mtu ambaye aliwaza hivyo miaka hiyo na kusema
atakuja kuzindua viatu vyenye uwezo wa kujifunga kamba. Na kwake ndoto
hio imetimia.
Wahandisi nchini Ujerumani wamebuni viatu ambavyo vina uwezo wa kujifunga kamba.
Walifanikiwa
kufanya hivyo kwa kuweka 'cherger'mfano kama ile ya simu kwenye viatu
hivyo ambavyo vinatumia kawi kujionea wenyewe itakavyokuwa kwenye miguu
tofauti.
Pindi unapovaa kiatu hicho, sensa ya kiatu inakiambia
kwamba mguu uko sawasawa na kuchochea kawi kwenye kiatu kile kuamrisha
kamba kujifunga zenyewe.
Wakati unataka kuvua viatu utahitajika
kubonyeza au kugonga wayo wa kiatu kile mara mbili na vile vile kuna
miale inayoamrisha kamba za viatu vile kujifungua kwa kuzilegeza kamba.
Wanasema
kiatu hicho hakihitaji kuwekwa kwenye charger au kubadilisha betri kwa
sababu kawi inatokana na hatua za kuukanyaga mguu chini kwa mvaaji au
anapotembea zile hatua ndizo zinakipatia kiatu nguvu au kawi.
Mmoja wa wahandisi waliokitengeza kiatu hicho, anasema kwamba kiatu hicho kitawasaidia watu wengi.
Miongoni
mwa watakaofaidi ni watu wanaokumbwa na ulemavu wa miguu au wenye
matatizo ya kutembea lakini pia vinaweza kuwasaidia watoto au kwa
wanaotaka tu kubadili mfumo wao wa maisha.
Saa moja ya kutumia viatu hivyo inatosha kuweza kurejesha kawi ya kufunga kamba.
0 comments:
Post a Comment