Mjadala
mkali umeingia siku ya pili nchini Tanzania kufuatia Rais wa nchi hiyo
Jakaya Kikwete kulihutubia taifa la nchi hiyo ambaye pamoja na mambo
mengine alitangaza kumfuta kazi waziri mmoja kwa kuhusika na kashfa ya
uchotaji wa mamilioni ya fedha kwenye account ya Escrow.
Upande wa
upinzani umekosoa hotuba hiyo na kusema alipaswa kutangaza kuwafuta
kazi mawaziri na watendaji wengine waliotajwa kwenye azimio la bunge
lilipelekwa kwake hivi karibuni.Wakati haya yakiendelea wahisani
waliositisha misaada kufuatia kashfa hiyo leo wamesema wamepokea kwa
furaha hotuba hiyo na wametangaza kuanza kuipata Tanzania fedha asilimia
15 ya walizoahidi kwenye bajeti.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
alitangaza kumfuta kazi waziri wa Ardhi Prof Anne Tibaijuka katika
hotuba yake hapo jana ambaye ni mmoja ya mawaziri wanaodaiwa kuhusika na
kashfa ya ufisadi ya kuhamisha isivyo halali fedha kwenya akaunti ya
Tegeta Escrow.Hotuba hiyo Rais Kikwete tangu jana imezua mjadala mkali
nchini Tanzania ambao wengi wamekuwa na maoni tofauti.
Chama Kikuu
cha upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimekosoa hotuba
hiyo na kusema kimesikitishwa na hatua alizozitangaza Rais Kikwete hapo
jana.Hivi karibuni Bunge la Tanzania liliapitisha maazimio nane ambapo
miongoni mwa maazimio hayo ilikuwa ni pamoja na serikali kuwachukulia
hatua ZA kinidhamu pamoja na kuwafuta kazi mawaziri na maafisa wa
serikali waliohusika katika sakata hilo.
Miongoni wa watendaji hao
ni Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo Katibu Mkuu wa
Wizara Eliakim Maswi, Waziri wa Ardhi, Profesa Anne Tibaijuka ,Bodi ya
Shirika la Umeme Tanzania Tanesco pamoja na maafisa wa na watendaji
wengine waliohusika kwa namna moja au nyingine katika sakata hilo.
Hata
hivyo katika hotuba hiyo Rais Kikwete mbali kumfuta kazi waziri huyo
mmoja wa Ardhi hakusema kama hao waziri mwingine aliyebaki ambaye ni
Waziri wa Nishati na Madini na Katibu Mkuu wake watachukuliwa hatua za
kinidhamu lini zaidi ya kusema anamweka kiporo waziri huyo huku
akisubiri uchunguzi dhidi ya waziri huyo jambo linalopingwa na upande wa
upinzani.
Wakati hayo yakiendelea nchi wahisani wa nchi zipatazo
12 ambazo zilisitisha misaada ya takribani dola milioni 500 kwenye
bajeti ya Tanzania zimesema kupitia kwa Mwenyikiti wao ambaye balozi wa
Finland nchini Tanzania Sinikka Antila zimesema kwa njia ya barua pepe
kwa BBC kuwa nchi hizo zimefurahishwa na hotuba ya Rais Jakaya Kikwete
kwa jinsi alivyokubali kutekeleza maazimio ya Bunge na kusema kuwa
kuanzia kuanzia leo wamekubali dola bilioni 84 sawa na asilimia 15 ya
mchango wao kwenye bajeti ya Tanzania.
Kwa upande mwingine upande
wa chama kinachotawala CCM kupitia kwa Katibu Mwenezi wa vijana wa chama
hicho Paul Makonda amesema wanaipongeza hotuba ya Rais Kikwete na hatua
alizochukua.
0 comments:
Post a Comment