KATIKA
kuhakikisha kuwa kunakuwepo na Ubora na Usalama wa dawa kwa matumizi ya
binadamu, Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini-TFDA, imefuta usajili na
kuzuia uingizaji, usambazaji na matumizi ya aina tano za dawa za
binadamu.
Akizungumza na Wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo HIITI SILLO, amesema kuwa uamzi huo
uliochukuliwa ni kutokana na matokeo ya mfumo wa ufuatiliaji na kubaini
uwepo wa dawa duni kwenye soko.
Bwana SILLO amezitaja baadhi ya dawa zilizofungiwa na Mamlaka hiyo
kuwa ni pamoja na dawa ya kutibu fangasi ya vidonge na dawa ya kutibu
malaria ya maji na Vidonge.
0 comments:
Post a Comment