UMOJA wa katiba ya
wananchi -UKAWA, umesema kuwa hawatashiriki katika mchakato wa kura za
maoni kutokana na mapungufu mbalimbali yanayolikabili zoezi hilo ikiwemo
mchakato wa kupata katiba pendekezwa haukuzingatia maridhiano ya
kitaifa.
Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa umoja huo ambaye ni
Mwenyekiti wa chama cha wananchi Cuf Profesa Ibrahim Lipumba amesema
kuwa kutokana na mapungufu hayo Ukawa walisusia mchakato huo tangu
ulipoanza na pia Rais alipuuza makubakubaliano baina ya umoja wa
Demokrasia Tanzania ambao unaundwa na vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni kuahirisha mchakato wa kura ya maoni hadi baada ya uchaguzi mkuu.
0 comments:
Post a Comment