KATIKA kutekeleza moja
ya malengo ya Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
kupitia Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Nchini Dubai katika Falme za
Kiarabu, umefanikiwa kulishawishi Shirika la Ndege la Emirates kuajiri
Watanzania kwenye Shirika hilo.

Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Simba Yahaya ameyasema hayo leo jijini
Dar es salaam, alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ambapo
amefafanua kuwa kupitia wandishi hao, Watanzania wenye sifa wataweza
kufahamishwa juu ya fulsa za ajira katika Shirika hilo na kutuma maombi
ya kazi.
0 comments:
Post a Comment