Hatimaye
leo wananchi wa Zambia wanapiga kura kuchagua Rais wa nchi hiyo,
kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Michael Sata Oktoba mwaka jana.
Chama
tawala cha Patrioyoc Front kinauhakika wa kushinda katika uchaguzi huo
licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka upinzani.
Waangalizi
wa kikanda katika uchaguzi huo, wanasema wameridhishwa na maandalizi ya
zoezi zima la upigaji kura.Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa na upinzani
mkali kati ya Edgar Lungu anayegombea nafasi hiyo kupitia chama tawala
na mpinzani wake HAKAINDE Hichilema kutoka United Party for National
Development.
Wagombea wote katika nafasi hiyo ya Urais wakati
wakijinadi wameahidi kuimarisha mfumo wa elimu nchini humo, kutengeneza
ajira. Huku wapiga kura nao wakitumaini kuwa wanasiasa hao watatimiza
ahadi zao.Ikiwa ni miaka 50 toka nchi hiyo ilipojipatia uhuru, Zambia
imekuwa imara na imeendelea na msimamo wake wa kufanya uchaguzi tangu
kumalizika kwa siasa za chama kimoja nchini humo.
Hata hivyo
mshindi katika uchaguzi huo wa leo atatumikia kipindi cha miezi 18
iliyobakia, katika awamu iliyobaki, aliyoiacha marehemu Michael Sata,
wakati nchi hiyo ikijiandaa kufanya uchaguzi mkuu mwakani 2016.
0 comments:
Post a Comment