Serikali
ya Uganda imeondoa ada ya kibali cha kufanyia kazi nchini humo pamoja
na mahitaji ya viza miongoni mwa raia wa Kenya na Rwanda wanaoingia na
kutoka taifa hilo.
Uamuzi huo uko sambamba na uidhinishaji wa
mtindo wa uhuru wa kutembea chini ya Itifaki ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki ya Soko la pamoja ambayo iliafikiwa mwaka 2009 na marais
Museveni wa Uganda,Mwai Kibaki wa Kenya na Jakaya Kikwete wa
Tanzania,Paul Kagame wa Rwanda na Pierre Nkurunziza wa Burundi.
Kamishna
wa udhibiti wa uhamiaji katika wizara ya maswala ya ndani bwana Anthony
Namara ameliambia gazeti la Monitor jumamosi kwamba raia wa mataifa
hayo mawili pia hawatahitajika kutoa viza ama vibali vyovyote vya
usafiri ili kuingia Uganda isipokuwa vitambulisho vyao pekee.
Amesema
kuwa Kenya na Rwanda tayari zinaidhinisha mpango huo wa uhuru wa
kutembea ambao unalenga kuimarisha utalii katika eneo hili mbali na
kuruhusu usafiri wa wataalam katika mataifa haya matatu.
0 comments:
Post a Comment