Wanaharakati nchini Afrika Kusini wameipa muhula wa siku 10 pekee
serikali ya nchi hiyo kuhakikisha inamtimua balozi wa utawala wa
Kizayuni wa Israel katika nchi hiyo. Taarifa ya pamoja iliyotolewa na
jumuiya tofauti za kiraia nchini humo imesema iwapo serikali ya Pretoria
haitasikiliza amri hiyo ya kumfukuza Arthur Lenk, balozi wa Israel
nchini mwao, basi watavamia majengo ya ubalozi wa utawala huo wa
Kizayuni na kumuondoa kwa nguvu. Pendekezo hilo la wanaharakati wa
Afrika Kusini limetolewa kufuatia pingamizi la viongozi wa Israel la
kumzuia Blade Nzimande, Waziri wa Elimu ya Juu wa Afrika Kusini kufanya
safari katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Jumuiya za
kiraia zilitoa taarifa hiyo jana, katika kikao kilichokuwa kimeitishwa
kwa lengo la kuchunguza utendaji wake ambapo pia washiriki waliitaja
hatua ya utawala wa Kizayuni ya kumzuia Nzimande na maafisa wengine
watatu wa Afrika Kusini kuingia ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa
mabavu, kuwa si tu kwamba ni kumdhalilisha waziri huyo, bali pia ni
kuudhalilisha udiplomasia wa Afrika Kusini na wananchi wote wa nchi
hiyo.
Afrika kusini ni moja kati ya nchi ambazo zimewapiga marufuku
wanafunzi wa Israel kujiunga na vyuo vikuu vya nchi hiyo, katika kupinga
na kulalamikia jinai za Tel-Aviv dhidi ya Wapalestina hususan wakazi wa
Ukanda wa Gaza
0 comments:
Post a Comment