Maandamano
yanaendelea kwenye mji mkuu wa Burundi Bujumbura kwa siku ya tatu
kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu.
Watu wanachoma magurudumu ya magari na kuweka vizuizi huku nao polisi wakirusha vitoa machozi.
Maandamano
hayo kwa mara ya kwanza, yamesambaa kwenda nje ya mji mkuu. Polisi
wamezuia wanafunzi wa chuo kikuu kwenye mji ulio kati kati mwa nchi wa
Gitega waliojaribu kuandamana kwenda mjini.
Umoja wa Mataifa
unasema kuwa karibu watu 25,000 wamekimbia nchi hiyo ndani ya majuma
mawili yaliyopita, wakihofia kuongezeka kwa ghasia kabla ya uchaguzi
mkuu unaokuja.
0 comments:
Post a Comment