Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amesema kuwa mashambulizi ya Saudi Arabia na waitifaki wake
huko Yemen yameidhalilisha nchi hiyo kimataifa. Akizungumza katika
hotuba ya Sala ya Ijumaa ya leo hapa Tehran, Hujatul Islam wal Muslimin
Kadhim Siddiqi ameashiria matukio ya Yemen na kusisitiza kuwa: Saudi
Arabia imezitumia rasilimali adhimu za umma wa Kiislamu kuishambulia
nchi ambayo haijafanya uvamizi wowote kwa nchi nyingine, bila kujali
sheria za kimataifa na hivyo kuvuruga amani ya eneo kwa kusaidiwa na
nchi kadhaa za Kiarabu ambazo zinadhibitiwa na madola yenye nguvu
duniani. Hujatul Islam wal Muslimin Siddiqi amesema kufanya uvamizi wa
wazi dhidi ya Yemen ni pigo kubwa la kisiasa kwa nchi inayojidai kuwa ni
ya Kiislamu na kueleza kuwa Saudi Arabia haiheshimu haki zozote za
Waislamu katika hali ambayo inajiarifisha kuwa hadimu wa Haramu mbili
Tukufu yaani Makka na Madina.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mji wa
Tehran ameashiria pia hatua ya Saudia ya kutumia silaha za kemikali
katika uvamizi wake wa kijeshi nchini Yemen na kusisitiza kuwa: Utawala
wa Aal Saud hadi sasa haujafanikiwa kufikia hata lengo lake moja na
katika siku za usoni pia nchi hiyo itashindwa kufikia malengo yako huko
Yemen. Katika hotuba ya Sala ya Ijumaa ya hapa Tehran, Imam wa Sala hiyo
ameashiria vile vile mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1
na kusema kuwa kuna udharura wa kuheshimiwa mistari myekundu kwenye
mazungumzo hayo.
0 comments:
Post a Comment