Polisi ya Thailand imetangaza kugunduliwa kaburi la umati ambalo
linasaidikiwa kuzikwa ndani yake Waislamu wa Myanmar waliokimbilia
nchini humo kwa ajili ya kuokoa maisha yao. Kwa mujibu wa maafisa
usalama, kaburi hilo limefichuliwa katika mji wa Songkhla, kusini mwa
nchi hiyo na ndani yake walizikwa wahajiri kutoka Myanmar na Bangladesh
wengi wao wakiwa ni Waislamu. Polisi ya Thailand imewalaumu
wafanyabiashara ya magendo ya watu kuwa ndio wahusika wa jinai hiyo.
Aidha imefichua kuwa, kaburi hilo limepatikana karibu na mpaka na nchi
jirani ya Malaysia na lipo ndani ya kambi ya kuhifadhia wahajiri ambayo
pia ilikuwa ikitumiwa kama jela katika siku za nyuma. Thailand ni moja
ya nchi zinazokandamiza sana Waislamu ikiwemo kuwapiga marufuku wanawake
wa Kiislamu kuvaa vazi la staha la hijabu mashuleni. Hata hivyo
ukandamizaji na unyanyasaji wa Wathailand ambao wengi wao ni Mabudha,
haukomei kwa Waislamu pekee wa nchi hiyo, bali hata Waislamu wa nchi
nyingine hususan kutoka Myanmar na Bangladesh hawakusalimika na
unyanyasaji huo wa viongozi wa Thailand.
0 comments:
Post a Comment