Jeshi la polisi
mkoani Iringa limekamata mikanda ya DVD yenye mafunzo ya kijeshi
yanayohusiana na kikundi cha ugaidi cha Al shaabab cha nchini Somalia
zilizokuwa zikitumika na watoto wa mitaani wanaodaiwa kuwa walikuwa
wakichukua mafunzo kwakutumia DVD hizo.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhan Mungi ametoa taarifa hiyo mbele ya
waandishi wa habari akieleza kuwa mikanda hiyo iliyokuwa ikitumiwa na
vijana hao wanne wenye umri kati ya miaka 12 na 16 inaonesha ukatili na
mauaji yanayodaiwa kufanywa na kikundi cha kigaidi cha Al
shaabab.Mikanda hiyo walikuwa wakiitazama kwa kutumia kompyuta mpakato
yaani laptop.
Aidha kamanda
Mungi amesema pamoja na mikanda hiyo ya DVD pia jeshi hilo limekamata
watu wawili wanaojihusisha na biashara ya bangi wakiwa na magunia matatu
ya bangi katika harakati za kufunga bangi hiyo kwenye vifurushi vidogo
tayari kuisambaza kwa wateja wao.
Mungi ameongeza
kuwa kamata kamata hiyo iliyofanywa na jeshi hilo mkoa wa Iringa pia
imekamata nguzo 35 za umeme za shirika la umeme nchini TANESCO, nyaya za
kusambaza umeme na vifaa vingine zikiwa zimehifadhiwa kwa watu binafsi
wawili ambao hakuwataja majina kwa sababu za kiupelelezi
0 comments:
Post a Comment