Meli iliyomatwa huko Glosgow |
Watu wawili raia wa Uturuki walionaswa mwaka
jana kwenye ufukwe wa Aberdeen, Scotland na meli iliyokuwa imebeba tani
tatu za dawa za kulevya aina ya cocaine huku ikiwa na usajili wa nchini
Tanzania, wamekutwa na hatia mahakamani nchini Scotland.
Mahakama Kuu ya Glasgow, mji mkuu wa Scotland imewakuta na
hatia watu hao ambao ni Mumin Sahin na Emin Ozmen kwa kukutwa na dawa
hizo za kulevya daraja A zenye thamani ya Paundi milioni 500 za
Uingereza ambazo ni sawa na Shilingi trilioni 1.49 za Tanzania. Aidha
mahakama hiyo haikuwakuta na hatia washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo
ambao ni, Kayacan Dalgakiran, Mustafa Guven, Umit Colakel na Ibrahim
Dag. Kwa mujibu wa habari hiyo, dawa hizo za kulevya tani 3.2 aina ya
cocaine na zilifichwa ndani ya meli ya MV Hamal iliyokuwa inapeperusha
bendera ya Tanzania. Inaarifiwa kuwa, kabla ya hapo meli hiyo,
inayomilikiwa na kampuni ya Kiev Shipping and Trading Corporation,
ilitia nanga kwa muda nchini Guyana, Amerika ya Kusini ambayo hutumiwa
kupakia cocaine kuelekea Amerika Kaskazini na Ulaya. Taarifa zaidi
zinasema kuwa meli hiyo iliyokamatwa Aprili 23, mwaka jana, ilikuwa
imetia nanga maili 100 kutoka ufukwe wa Aberdeen, Uingereza baada ya
kuzuiwa kuingia nchini humo. Hiyo ni meli ya tatu kukakamatwa ikiwa
imebeba mzigo mkubwa wa dawa za kulevya baada ya ile iliyokamatwa nchini
Italia ikiwa na usajili wa Tanzania ikiwa na tani 30 za cocaine na
nyingine ya Canada iliyokamatwa katika Bahari ya Hindi nchini Tanzania
ikiwa na kilo 283 za cocaine.
0 comments:
Post a Comment