Na Chibura Makorongo, Kahama
Mwanafunzi
wa darasa la tatu katika shule ya msingi Majengo wilayani Kahama mkoani
Shinyanga, Said Joshua (12) amenusurika kufa baada ya baba yake mzazi
kujaribu kumchinja, kutokana na kile kinachodaiwa kuchoshwa na kumtibu
mtoto huyo maradhi ya muda mrefu..
Tukio
hilo limetokea jana saa 11 alfajiri katika kijiji cha Majengo, kata ya
Majengo, tarafa ya Kahama mjini ambapo mwanamme aitwaye Joshua Salvatory
(37) mkazi wa Majengo,fundi baiskeli akiwa nyumbani kwake alimkata kisu
shingoni mtoto huyo na kuathiri koromeo lake.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya Kahama mkoni Shinyanga,Dkt Joseph Fwoma
alisema mtoto huyo alifikishwa hospitalini hapo baada ya kuokotwa na
wasamaria wema huku akivuja damu nyingi shingoni.
Dkt
Fwoma alisema baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini madaktari
walimfanyia upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo aliyochinjwa na hali
yake inaendelea vizuri hasa baada ya kuongezwa damu.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo Mariamu Idd (35) alisema, mtoto wake alichukuliwa na baba yake mzazi siku moja kabla ya tukio na kwenda naye kwake eneo la Majengo mjini Kahama anakokaa.
“Nimepigiwa simu na kuelezwa taarifa za kuchinjwa kwa mwanangu na baada ya tukio baba wa mtoto amekimbilia kituo cha polisi Mjini Kahama kujisalimisha”,alieleza mama wa mtoto huyo.
“Baba wa mtoto huyu siku za nyuma,alikuwa akimchukua mwanangu mara kwa mara na kumpeleka nyumbani kwake,mimi nilishaachana naye, huwa anamrudisha,na amekuwa akidai kuchoshwa na huduma za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na matatizo ya kiafya”,alifafanua mama huyo.

Jeshi
la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo,
ambapo, kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla
alisema chanzo cha tukio hilo kinasadikiwa kuwa mtuhumiwa anaugua
ugonjwa wa akili.
Wakati
huo huo mtoto wa kiume (miezi 6) asiyefahamika jina wala makazi yake
amekutwa kichakani akiwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa hauna
jeraha na ukiwa tayari umeanza kuharibika.
Kamanda
Mangalla alisema tukio hilo limetokea Machi 4, mwaka huu saa 12 jioni
katika kijiji na kata ya Mhongolo wilayani Kahama na kuongeza kuwa
inaonesha mtoto huyo alitupwa katika siku tatu zilizopita.
Alisema
chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa huku akiwataka wananchi
kushirikiana na jeshi la polisi ili kumbaini na kumkamata mtuhumiwa
aliyetupa mtoto huyo.
0 comments:
Post a Comment