Wakati utata wa kuchotwa kwa fedha katika Akaunti ya Escrow iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na mgogoro baina ya IPTL na Tanesco ukiendelea kuzua maswali, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema fedha hizo hazikuwa za Serikali.
“Hizo fedha hazikuwa za Serikali, Tanesco ilitakiwa kulipa Capacity
Charge (gharama za uwekezaji) kwa IPTL kama inavyolipa karibu Sh27
bilioni kwa kampuni nyingine zinazozalisha umeme,” alisema Profesa
Muhongo.
Itakumbukwa kuwa, kutokana na mgogoro wa IPTL na Tanesco
akaunti hiyo ilifunguliwa ili fedha ambazo Tanesco ilipaswa kuilipa
IPTL kwa ajili ya Capacity Charge ziwekwe kwenye akaunti hiyo hadi
mgogoro huo utakapomalizika.
Kwa kuwa malalamiko yalikuwa kwamba, fedha ambazo Tanesco ilikuwa
ikiilipa IPTL zilikuwa nyingi kuliko ilivyostahili, ilitarajiwa kwamba
baada ya kesi iliyofunguliwa Marekani kuamuriwa, ingepatikana njia
kukokotoa gharama halisi na sehemu ya fedha hizo kurudi Tanesco.
Sehemu ya taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano Tanesco
Makao Makuu, Jumanne iliyopita kufafanua taarifa zilizokuwa zimeandikwa
juu ya hukumu hiyo inasema: “Mahakama hiyo (ya Kimataifa ya Usuluhishi
wa Migogoro ya Uwekezaji) haikutangaza aliyeshinda wala kushindwa.
“Ilichofanya ni kutoa muda wa miezi mitatu kwa pande zote mbili,
(Standard Charted Bank Hong Kong (SCB-HK)) na Tanesco kwenda kukubaliana
nje ya Mahakama… kwa sasa kuna mazungumzo yanayoendelea kuhusu taratibu
za kukokotoa gharama halisi.
“Hivyo basi, kanuni itakayokubaliwa na pande hizo mbili ndiyo
itakayosema SCB-HK alipwe kiasi gani ambapo ilitarajiwa angelipwa
kupitia fedha zilizokuwa Escrow.”
Profesa Muhongo alipoulizwa iwapo Serikali inaitambua SCB- HK na
hukumu iliyotolewa na Mahakama hiyo ya Kimataifa, alisema kwa kifupi:
“Kwani sisi tunaendeshwa na sheria za Marekani? Je, hao wabia wengine
wanamtambua SCB-HK?”
Pia hakutaka moja kwa moja kukiri kuwa Serikali ndiyo iliyotoa fedha
hizo na kuzitoa kwa Pan African Power Solution wala kukanusha taarifa
hizo, badala yake alisema swali hilo waulizwe wahusika katika suala
hilo.mwanachi
0 comments:
Post a Comment