CHELSEA NJE ULAYA, YAPIGWA 3-1 DARAJANI...FAINALI NI ATLETICO NA REAL MADRID
CHELSEA
imeaga Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufungwa mabao 3-1 na Atletico
Madrid ya Hispania usiku huu Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Atletico
sasa itakutana na jirani zao, Real Madrid katika fainali mwezi ujao
nchini Ureno, ambao jana waliwang’oa mabingwa watetezi, Bayern Munich
kwa 4-0 mjini Munich na kufanya ushindi wa jumla wa 5-0.
Fernando
Torres alitangulia kuifungia Chelsea dakika ya 36 kwa pasi ya
Azpilicueta baada ya kazi nzuri ya Willian, lakini Adrian Lopez
akaisawazishia Atletico dakika ya 44 kwa pasi ya Juanfran.
Diego
Costa akafunga bao la pili kwa penalti dakika ya 61 kabla ya Arda Turan
kumaliza kazi dakika ya 72 na Atletico imefuzu kwa ushindi wa jumla wa
3-1 baada ya sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza Madrid wiki iliyopita.
Mabadiliko
yaliyofanywa na kocha Jose Mourinho dakika ya 54 kumtoa beki Ashley
Cole na kumuingiza mshambuliaji Samuel Eto’o ndiyo yaliigharimu Chelsea.
Eto’o ndiye aliyesababisha penalti iliyofungwa na Costa.
Kwisha kazi; Mfungaji wa bao la tatu la Atletico Madrid, Arda Turan akishangilia |
0 comments:
Post a Comment