Mjadala umezuka nchini Rwanda
ambapo baadhi ya wananchi wanataka kurejeshwa kwa hukumu ya kifo nchini
kufuatia kesi dhidi ya mwanamme mmoja, mtumishi wa nyumbani,
anayetuhumiwa kumuua mtoto wa kike kwa kumkata kichwa.
Rwanda haina hukumu ya kifo na baadhi ya
wananchi wameelezea haja ya serikali kufanya marekebisho ya sheria ili
kuirejesha hukumu hiyo.Mamia ya watu walijitokeza kwenye uwanja wa michezo wa Nyamirambo kushuhudia kesi iliyofanywa hadharani kwa mara ya kwanza.
Mamia ya watu walijitokeza kusikiliza kesi inayomkabiliwa Sylivester Hola, ambaye alimuua msichana mwenye umri wa miaka 12, aliyekuwa binti wa mwajiri wake, ambaye amemfanyia kazi zaidi ya miaka 10.
Maafisa wa polisi walikuwa na muda mgumu kujaribu kuwazuia watu waliotaka kumwadhibu mtu huyo wenyewe.
Raia mmoja wa Rwanda, ambaye hakutaka jina lake kutajwa aliiambia BBC kuwa hukumu ya kifo ni sharti irejeshwe:
"mtu anayeua kwa kisu anapaswa kuuawa kwa risasi au apigwe risasi na auwawe ili uwe mfano kwa watu wengine kama yeye," mtu huyo alisema.
0 comments:
Post a Comment