ASKARI Polisi wanne wa kituo cha Polisi Singida mjini na wakazi
15 wa kijiji cha Utaho tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi mkoani
Singida,wamefariki dunia baada ya kugongwa na basi la kampuni ya summry
T.799 BET aina ya nissan.
Tukio hilo limetokea Aprili 28 mwaka huu saa 2.45 usiku katika
barabara kuu Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Utaho wilaya ya Ikungi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida,SACP.Geofrey
Kamwela askari hao ni F.849 D/CPL Boniface Magubika,F.6837 Pc Jumanne
Mwakihamba,G.7993 Pc Novatus Tarimo na G.8948 Pc Michael Mwakihaba.
Alitaja wengine waliofariki kuwa ni pamoja na Ramadhani Mjengi
afisa mtendaji wa kijiji cha Utaho,Paul Hamisi mwenyekiti wa kijiji cha
Utaho,Ernest Salanga,mwenyekiti wa kitongoji cha Utaho,Saidi
Rajabu,Usirika Itambu,Chima Mughenyi,Slim Juma,Abeid Ramadhani,Mwinyi
Hamisi na Issa Husein wote wakazi wa kijiji cha Utaho.
Aidha,Kamwela amesema kuwa miili ya watu wengine bado
haijatambuliwa na imehifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha hospitali ya
mkoa mjini Singida.
Akizungumuzia juu ya ajali hiyo,kamanda huyo amesema kuwa awali
kijana Gerard Zephania (24) akiwa ametoka kusaga nafaka aligongwa na
gari la mizigo ambalo bado halijafahamika na kufariki papo hapo.
“Askari wa polisi wakitumia gari PT 1424,walifika eneo la tukio kwa
ajili ya kuubeba mwili wa Gerard kuuleta katika hospitali ya mkoa kwa
uchunguzi,kundi la wananchi wa kijiji cha Utaho nao walifika eneo la
tukio”,amesema na kuongeza;
“Wakati askari polisi wakiwa kwenye harakati ya kuupakia mwili huo
ghafla basi la summry liliacha njia na kuingia kushoto mwa barabara kwa
nia ya kulikwepa gari la polisi na ndipo lilipovamia na kugonga kundi la
watu hao wakiwemo askari polisi.Watu 15 walifariki papo hapo”,amesema
Kamwela.
Kamanda Kamwela amesema kuwa dereva wa basi hilo Paulo Njilo mkazi
wa Dar-es-salaam hakuweza kusimamisha basi hilo nadi kilomota 25
alipolisimamisha na yeye kutorokea kusikojulikana.
Aidha,amesema ajali hiyo imesababisha majeruhi nane ambapo wawili
kati yao wamelazwa katika hospitali ya mkoa na hali zao zinaendelea
vizuri.Majeruhi wengine sita wamelazwa katika hospitali ya misioni ya
Puma na hali zao sio nzuri.
“Uchunguzi zaidi juu ya ajali hiyo unaendelea ili kujua chanzo
halisi cha tukio pamoja na kumtafuta dereva wa basi ili aweze kuhojiwa
na kisha hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake”,amesema
Kamanda Kamwela.
Baadhi ya ndugu wakiwa nje ya chumba cha kuhifadhia maiti cha
hospitali ya mkoa mjini Singida,wakisubiri kuchukua miili ya ndugu zao
waliogongwa na basi la Summry.
Baadhi ya ndugu na jamaa wakiwa wanatafakari juu ya ndugu zao
kugongwa na basi la summry la kufariki dunia usiku wa kuamkia leo katika
kijiji cha Utaho wilaya ya Ikungi.
Basi la Summry liliua watu 18
Gari la polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa
hospitali ya mkoa wa singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa
Moja ya maiti ya ajali ya basi la sumry iliyo tokea katika kijiji cha
Utaho Wilayani Ikungi ikisubiri kupakiwa katika gari la polisi.
0 comments:
Post a Comment