Jarida la The Voice la nchini Uholanzi limemtangaza Rais Jakaya
Kikwete wa Tanzania kuwa mshindi wa tunzo ya demokrasia mwaka 2014.
Tangazo hilo limetolewa na kamati maalumu ya jarida hilo inayohusika na
kuandaa tunzo hiyo. Kwa mujibu wa kamati hiyo, Rais Kikwete ameshinda
baada ya kuwabwaga washindani wengine wawili ambao majina yao
hayakutajwa. Taarifa zaidi zinasema kuwa, Rais Kikwete ameteuliwa
kutokana na mchango wake wa kukuza demokrasia ndani ya nchi yake
sambamba na kutetea utawala bora barani Afrika. Azma yake ya kuhakikisha
Tanzania inapata Katiba mpya ni sababu nyingine iliyochangia ushindi
wake. Rais wa Tanzania anakuwa kiongozi wa pili aliyeko madarakani
kushinda tunzo hiyo tangu ilipoanzishwa na anatarajiwa kupokea rasmi
tunzo yake mwezi Septemba mwaka huu kwenye hafla maalumu huko Uholanzi.
Mwaka uliopita, Rais wa Sierra Leone, Earnest Bai Koroma ndiye
alyetunukiwa tunzo hiyo. Rais wa zamani wa Zambia, Kenneth Kaunda ndiye
aliyekuwa mshindi wa tunzo hiyo mwaka 2012. Mwezi Aprili mwaka huu,
Rais Jakaya Kikwete pia alishinda tunzo nyingine ya kimataifa kuhusiana
na masuala ya utawala bora.
0 comments:
Post a Comment