Watu wasiopungua 16 wamepoteza maisha yao mjini Benghazi Libya
kufuatia mapigano kati ya jeshi la nchi hiyo na wanamgambo wanaoipinga
serikali. Duru za hospitali na za kijeshi zimetangaza kuwa, wahanga
wengi wa mapigano hayo ni wanajeshi. Aidha miongoni mwa waliouawa wapo
raia watatu mmoja wao akiwa ni raia wa Misri, ambao walipoteza maisha
yao baada ya nyumba yao kushambuliwa na kombora. Taarifa zaidi zinasema
kuwa, watu 81 wamejeruhiwa katika mapigano hayo. Mapigano hayo yalizuka
jana baada ya wanamgambo hao kushambulia kambo ya jeshi. Mauaji hayo
yametokea siku moja tu baada ya watu 47 kuuawa mjini Tripoli kwenye
mapigano makali yaliyotokea kati ya makundi ya wanamgambo hasimu
wanaopambana nchini Libya. Mapigano hayo yalijiri wakati makundi hayo
yalipokuwa yakipambana kwa shabaha ya kutaka kuudhibiti uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Tripoli, ulioko umbali wa kilomita 25 kutoka mji mkuu wa
nchi hiyo.






0 comments:
Post a Comment