Mtoto aliyeuawa shahidi katika hujuma za Israel Ghaza
Idadi ya wahanga wa mashambulizi ya utawala haramu wa Kizayuni wa
Israel katika eneo la Ukanda wa Ghaza, imeongezeka na kupindukia watu
620. Kwa mujibu wa habari rasmi zaidi ya watu 40 wameuawa shahidi hii
leo katika maeneo tofauti ya ukanda huo hususan katika maeneo ya Hai
Zaitun na Beit Hanun. Moja ya wahanga wa jinai hizo za Wazayuni ni mtoto
mwenye umri wa miezi minne. Hii ni katika hali ambayo Brigedi ya
Izzudin Qassam tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya
Palestina HAMAS imetangaza kuwaangamiza askari 52 wa Kizayuni akiwemo
kamanda wa ngazi za juu wa jeshi la Israel, katika mapigano ya ana kwa
ana tangu utawala huo pandikizi ulipoanzisha mashambulizi yake katika
eneo hilo. Mbali na askari hao 52, wanamapambano hao wa Palestina,
wamesambaratisha magari ya deraya yapatayo 36 na vifaru saba. Wakati huo
huo Katibu Mkuu wa Mpango wa Ubunifu wa Kitaifa wa Palestina Mustafa
Barghuthi amesisitiza kuwa hakutakuwa na usitishaji vita maadamu adui
Mzayuni bado anaendelea kuuzingira eneo la Ghaza. Barghuthi ameyasema
hayo hii leo na kuongeza kuwa, ni miaka minane sasa wakazi wa ukanda huo
wanateseka kwa matatizo mbalimbali na kwamba umewadia wakati wakazi hao
waishi kwa heshima na utukufu. Aidha amesema kuwa, utawala haramu wa
Kizayuni hauheshimu makubaliano yoyote unayofikia na Wapalestina.






0 comments:
Post a Comment