Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limefichua kuwa, Tzipi
Livni, Waziri wa Sheria wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel,
amenusurika kuangamia baada ya kuanguka karibu yake kombora la
wanamapambano wa Kipalestina jana jioni huko katika ardhi za Palestina
zinazokaliwa kwa mabavu. Kwa mujibu wa gazeti hilo, Livni alikumbwa na
wahka mkubwa, licha ya kwamba hata hakujeruhiwa. Livni amenusurika
wakati alipokuwa anatembelea moja ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni
karibu na Ukanda wa Ghaza. Baada ya tukio hilo, waziri huyo wa sheria wa
utawala pandikizi wa Kizayuni aliondoshwa haraka katika eneo hilo na
kukatisha kabisa shughuli hiyo. Hii ni katika hali ambayo utawala huo
haramu umekiri kuuawa na kujeruhiwa idadi kubwa ya Wazayuni wakiwemo
viongozi wandamizi. Muqawama wa Kipalestina umetangaza kuwa utawala huo
unaficha ukweli wa mambo kuhusiana na hasara unayopata utawala wa
Kizayuni katika vita vinavyoendelea hivi sasa kati ya pande mbili. Kwa
mujibu wa wanamapambano wa Kipalestina, wanamapambano hao jana pekee
waliwaangamiza askari wa Kizayuni 23 lakini utawala huo umeficha ukweli.






0 comments:
Post a Comment