Kesi
imeanza dhidi ya mwanamume anayedaiwa kumuua na kumkataka vipande
mpenzi wake mwanamume Jun Lin na kuwatumia wanasiasa vipande vya mwili
wake kupitia kwa njia ya posta.
Inaarifiwa pia alitumia baadhi ya vipande vya mwili wa mwanamume huyo kwa shule kadhaa nchini humo.
Luke
Magnotta mwenye umri wa miaka 32 alifikshwa mahakamani mjini Montreal
lakini alikanusha madai ya mauaji hayo yaliyotokea mwaka 2012.
Ikiwa atapatikana na hatia atafungwa maisha jela.
Mpenzi wa Magnota alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu raia wa China.
Polisi
walianza uchunguzi wa mauaji hayo, baada ya kupata kiwiliwili cha
mwanamume huyo karibu na nyumba ya Magnotta. Polisi walianza msako wa
kimataifa kumtafuta Magnotta na hatimaye kumkamatia katika duka huduma
za internet mjini Berlin Ujerumani.
Polisi walipata vipande vya mwili wa Lin katika posta vikiwa vimetumiwa waziri mkuu Stephen Harper pamoja na wasiasa wengine.
Polisi
pia walipata vipande vingine vikiwa vimetumwa kwa shule mbili za
kiingereza. Kicwa kilipatikana katika bustani la Montreal.
Kadhalika wachunguzi walipata video kwenye mtando ikionyesha mauaji ya Lin.
0 comments:
Post a Comment