BISMILLAH
RRAHMAN RRAHIM
TAARIFA MUHIMU KWA WAISLAM.
KUMEKUWA NA TAARIFA ZA KUWEPO MECHI YA MPIRA WA MIGUU KATI YA WANAOITWA
MASHEIKH WA KIISLAM NA WAKRISTO
MECHI HIO INATARAJIWA KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA MNAMO OCTOBER 12.
MADHUMUNI MAKUBWA YA YAMEELEZWA KUWA NI KUJENGA MSHIKAMANO KATI YA
WAISLAM NA WAKRISTO.
PAMOJA NA HAYO KUMEKUWA NA TAARIFA YA KUENDELEZA MECHI HIZO KWA UPANDE
WA WANAWAKE WA KIISLAM NA WALE WA KIKRISTO KATIKA KILA MKOA KATIKA
MCHEZO WA NETIBOLI NA KUFANYA MAANDALIZI YA MICHEZO MINGINE.
TUKIWA KAMA MUUNGANIKO WA VIJANA WA KIISLAM WA TANZANIA,NA BAADHI YA
NCHI ZA AFRIKA, ARABUNI ULAYA NA CANADA TUNAPENDEZA KUELEZA YAFUATAYO:
MECHI HIO HAINA.UHUSIANO WOWOTE ULE NA UISLAM KWANI HAIPO KATIKA
MAFUNDISHO YA UISLAM KWA SABABU ZIFUATAZO:
1.KATIKA MPIRA HUO HAKUTAKUWA NA UWEZEKANO WA KUZUIA MCHANGANYIKO KATI
YA WANAUME NA WANAWAKE PAMOJA NA VINYWAJI KAMA VILE POMBE NA VINGINEVYO
MAMBO HAYA YANAWEZA KULETE ATHARI KUBWA.
2.MUDA WA SWALA YA AL ASRI NA MAGHARIBI KATIKA HALI YOYOTE UTAINGILIANA
NA MPIRA HIVYO KUSABABISHA WASHIRIKI KUSHINDWA KUTEKELEZA AMA
KUTOTEKELEZA SWALA HIZO KWA MUDA MUAFAKA.
3.MAVAZI YATAKAYOVALIAWA NA NA WACHEZAJI WA PANDE MBILI AMA MOJAWAPO
HAYATAKUWA YANAZINGATIA SHERIA ZA KIISLAM.
4.MAUDHUI YA MCHEZO HUO HAYAKIDHI SHERIA ZA KUKUTANA KWA WAISLAM NA
WASIO WAISLAM MKUSANYIKO HUU UNA SURA YA "MFU" NA SI YA "MTU"
WITO KWA WAISLAM.
NIA KUBWA YA KUANDALIWA MCHEZO HUU NI KUTUANGALIA WAISLAM NAMNA GANI
TUMELALA ILI WAWEZE KUPITISHA AZMA NA MALENGO YAO MAOVU DHIDI YA WAISLAM
WA TANZANIA!!
SHIME KILA MZAZI AHAKIKISHE MTOTO WAKE WA KIUME AU WA KIKE HAHUDHURII
"MUNKARI" HUU KWANI ATAKWENDA KUULIZWA JUU YA HILI SIKU YA HUKUMU.
VIJANA HII DINI IPO MIKONONI KWETU NA DUNIA KWA SASA INAMTAZAMA KIJANA
WA KIISLAM,HIVYO TUTUMIE KILA TULICHONACHO NA TUNACHOWEZA KUZUIA
"MUNKAR" HUU KWANI TUKIKUBALI KULIRUHUSU HILI KUPITA TUTAKUWA TUMETOA
MWANYA KWA MENGINE ZAIDI YA HAYA.
KITENDO CHA ANAYEITWA SHEIKH WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUJIFANANISHA NA
MCHEZAJI WA MPIRA AMBAE NI KAFIRI KIMETUHUZUNISHA SANA.
TUNAMWAMBIA HUYO ANAYEITWA SHEIKH KUWA SISI KIIGIZO CHETU
(TUNAEJIFANANISHA NAE) NI MUHAMMAD BIN ABDILLAH (SWALLA LLAHU ALAHYI
WASAALAM)
YA ALLAH UMETUSHUHUDIA TUMEFIKISHA!
UJUMBE KUTOKA KIJIJI CHA QURAN NA SAYANSI.
0 comments:
Post a Comment