Timu ya Manchester United imekubali kumpa usajili wa kudumu mshambuliaji Radamel Falcao kwa ada ya uhamisho wa pound million 56.
Masharti ya mkataba yamesainiwa kwenye makataba wa uhamisho ambao utamplipa mchezaji huyo €305,000 kwa wiki, ambapo miamba hiyo ya Old Trafford inategemea kumaliza taratibu za uhamisho katika majira ya joto.
United wanamalizia masharti ya mkataba na mchezaji huyo wa Monaco ambaye kwa sasa anaichezea United kwa ada ya €8m ikiwa ni kwa mkopo wa mda mrefu, usajili uliofanyika siku ya mwisho ya usajili.
Wakala wa mchezaji Falcao, Jorge Mendes, ana uhusiano mkubwa na bodi ya club hiyo na mchezaji Falcao ameonesha nia yake ya kuendelea kukipiga klabuni hapo daima.
0 comments:
Post a Comment