pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Ndoa ya UKAWA Itavunjika - CCM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa ndoa ya vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) si tishio, kwani hizo ni porojo tu na haitaweza kudumu.
Akizungumza kwenye Baraza la mkoa la Jumuiya ya Wazazi mkoani Pwani, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Jackson
Josian alisisitiza kuwa muungano huo
hautadumu. Josian alisema kuwa wapinzani walioungana,hawataisumbua CCM kutokana na viongozi wao kutokuwa na ushirikiano, kwani kila mmoja anaangalia upande wake.
“Ndoa ya UKAWA haiwezi kudumu,kutokana na wapinzani kuwa watu wa vitisho tu na hawawezi kuongoza hata ndani ya vyama vyao,” alisema Josian. Alisema kipimo kizuri kilikuwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, ambapo walionesha udhaifu mkubwa kwa kususia, ambapo Katiba ndiyo mustakabali wa nchi yoyote.
“Wao wanaangalia maslahi ya vyama vyao, na si maslahi ya umma, kwani hata kama walikuwa na hoja za msingi wangepinga wakiwa ndani ya Bunge na siyo nje, hivyo hawa hawafai kupewa madaraka na ndoa yao haitutishi kwani itavunjika,” alisema Josian. Katibu wa CCM Kibaha Mjini, Abdallah Mdimu alisema kipindi hiki ni vita kuelekea
uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na
vitongoji. Mdimu alisema kuwa kwa sasa chama kiko kwenye mchakato wa kuwapata wanachama wenye sifa, watakaogombea katika uchaguzi
huo wa serikali za mitaa. Aliwataka wanachama kutowachafua baadhi
ya wagombea, kwani mamlaka ya kujua kuwa mgombea fulani hana sifa ni ya vikao, ambavyo vikao vya kisheria na si mtu kutoa maamuzi.

0 comments:

Post a Comment