SERIKALI
ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama
moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030
katika mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya
milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya,
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy
amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya
agenda za maendeleo.
“Tunatambua
haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata
katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake
lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy
Amesema
kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika
Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda
ya watanzania na si agenda ya maendeleo.
Balozi
Mushy aliongeza kwamba serikali ya Tanzania imeweka msimamo huo zaidi
hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete aliagiza hivyo kwa maofisa wa
Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Waziri husika kukataa shinikizo la
kukubali swala ushoga kama agenda za maendeleo.
Amesema
kwamba watanzania wanataka maswala yanayowagusa kama vile maji, elimu,
huduma bora za afya, miundombinu ya umeme, ajira, umaskini na kuondoa
umaskini wa kipato.
Balozi
Mushy alifafanua zaidi kwamba mambo ya ushoga na ndoa za jinsia
yanakwenda kinyume na maadili ya watanzania, maisha, historia,
utamaduni, mila na desturi za mtanzania sinakataza maswala ya ushoga.
Amesema
kwamba serikali inatambua kwamba sheria ya mwenendo wa makosa ya
kujamiiana yaliwekwa na mkoloni mwingereza kabla ya uhuru na serikali ya
Tanganyika imerithi kutoka kwenye serikali ya mwingereza.
0 comments:
Post a Comment