MFUNGAJI Bora wa Ligi Kuu Barammsimu uliopita, Amissi Tambwe, kwa sasa anaonekana si lolote katika timu yake ya Simba ambapo amefunga bao moja tangu msimu huu uanze lakini imebainika kuwa mfumo anaotumia kocha wao Patrick Phiri ndio chanzo cha kuporomoka kwa straika huyo. Mchezaji huyo ambaye ameanza kuwatamanisha baadhi ya viongozi wa usajili wa Yanga ametamka kwamba anamalizia mechi zake mbili zilizobaki Simba kufunga mwaka halafu arudi kwao Burundi ambako anaweza kufanya uamuzi mgumu kutokana na vitisho alivyopata klabuni kwake hivi karibuni. Habari za ndani zinadai Tambwe ambaye amebakiza miezi mitano katika mkataba wake ameanza kujadiliwa na baadhi ya vigogo wa Yanga ambayo tayari ina wachezaji watano wa kigeni, lakini mtihani ni jinsi ya kumshawishi kocha Mbrazili Marcio Maximo. Hata hivyo mabosi hao wanadai watajua cha kufanya baada ya kumaliza mechi zilizosalia mwaka huu na kusikia tathmini ya Kocha. Wakati Simba ilipokuwa chini ya kocha, Zdravko Logarusic, kocha huyo alikuwa hampi majukumu mengi Tambwe huku kazi yake kubwa ikiwa ni kukaa eneo moja na kusubiri mipira ya kufunga ambapo alikuwa kitumia mifumo ya straika mmoja mbele 4-5-1 au 4-2-3-1. Lakini Phiri amempa Tambwe majukumu mawili ambapo anashuka kutafuta mipira na kupanda kufunga jambo ambalo limekuwa gumu kwake kumudu majukumu mawili kwa wakatinmmoja Phiri hupendelea sana kutumia mifumo ya 4-4-2, 4-3-3 na 3-5-2. Tambwe alikiri kuwa mabadiliko hayo pia yamechangia kiwango chake kuonekana kushuka kwani hawezi kufanya yote hayo kwa wakati mmoja.
“Kila kocha ana mfumo wake wa ufundishaji, nilipokuwa chini ya Loga
sikuwa na majukumu mengi katika timu, lakini hivi ninapewa majukumu
mengi ambayo si rahisi kuyafanya kwa
wakati mmoja na kuleta mafanikio hivyo nalazimika kucheza kutokana na
kocha anavyotaka,” alisema Tambwe.
Tambwe pia ni miongoni mwa wachezaji wanaotuhumiwa kucheza
chini ya kiwango kutokana na matokeo
ya sare tano mfululizo huku akitajwa
kuwa ni mmoja wa wachezaji.watakaotemwa kwa kosa hilo ambapo
yeye amesema kwamba yupo tayari
kuondoka ili kupisha wengine watakaoisaidia Simba. “Nipo katika wakati mgumu sana kwa sasa, tuhuma zimezidi jambo ambalo si kweli, nakosa amani ndani ya timu hivyo sioni sababu ya kuendelea kuwepo sehemu ambayo maisha yangu yapo hatarini, maisha ya mpira ndivyo yalivyo lakini kwa sasa yamezidi maana imefikia hatua natumiwa ujumbe wa vitisho, sasa nasubiri nini Simba? Nataka nikapumzike kidogo,” alisema Tambwe
Tambwe pia alikuwa mfungaji bora katika michuano ya Kombe la Kagame
alipokuwa na timu yake ya Vital’O ya
Burundi 2013 yaliyofanyika Sudani
Kusini ambapo alifunga mabao sita.
Lakini Phiri, alisema hupenda kutumia
mifumo hiyo ili timu iweze kushambulia zaidi na kupata mabao, pia alikiri wachezaji wengi wameathirika kisaikolojia kutokana na matokeo wanayoyapata.
0 comments:
Post a Comment