Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amepuuza wasi wasi wa nchi za
Magharibi kutokana na kuchaguliwa kwake katika nafasi ya uenyekiti wa
Umoja wa Afrika na kusema kuwa, wasi wasi huo hauna umuhimu wowote
kwake. Rais Mugabe ameyasema hayo jana mjini Addis Ababa siku moja baada
ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika. Rais wa Zimbabwe
ameongeza kuwa siasa za madola ya Magharibi kuwawekea vikwazo viongozi
wa nchi zisizokubaliana na mienendo yao, ni jambo lisilokubalika kama
vile ambavyo hazina itibari yoyote. Rais Mugabe amesisitiza kuwa, kama
mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, atafanya juhudi kubwa kwa ajili ya kuinua
kiwango cha maisha ya Waafrika. Amefafanua kuwa, atatumia uwezo wake
wote katika kuhakikisha maamuzi chanya yanapasishwa na Umoja wa Afrika
kwa maslahi ya nchi za bara hilo. Ameongeza kuwa, AU itashirikiana na
nchi za Ulaya endapo tu nchi hizo zitaamiliana na umoja huo kwa nia
njema ya ushirikiano.
0 comments:
Post a Comment