Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran alasiri ya leo ameelekea Nairobi mji mkuu wa Kenya
akiongoza ujumbe wa maafisa kadhaa wa Iran. Katika safari yake huko
Kenya, Muhammad Javad Zarif atakutana na kufanya mazungumzo na waziri wa
Mambo ya Nje wa Kenya na maafisa wengine wa nchi hiyo. Pande mbili hizo
zitakuwa na mazungumzo yatakayojadili uhusiano wa Iran na Kenya,
masuala ya kieneo na kimataifa. Muhammad Javad Zarif pia atazitembelea
nchi za Uganda, Burundi na Tanzania. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
amesema kuwa, safari yake hiyo huko Kenya, Uganda, Burundi na Tanzania
inafanyika kuafutia mwaliko kutoka kwa mawaziri wenzake wa nchi hizo.
0 comments:
Post a Comment