MWANAMKE mmoja amekamatwa na raia wema katika Wilaya ya Bunda,
mkoani Mara, na kufikishwa katika kituo cha polisi baada ya kudaiwa
kumnyanyasa mtoto wa kambo wa miaka minne, kwa kumpiga na kumlisha
kinyesi chake kwa madai ya kujisaidia ndani ya nyumba yake.
Joyce Maneno, mkazi wa mtaa wa Idara ya maji katika mji huo,
alikamatwa na wananchi wa eneo hilo, baada ya kugundua kunyanyaswa kwa
mtoto huyo ambaye umchapa, umpiga, na kumlisha kinyesi chake.
Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bunda, Chiku Mshora, alikiri
kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa liliripotiwa polisi na mwanamke
huyo alikamatwa.
Alisema kuwa baada ya muda mwanamke huyo alidhaminiwa na kutoka huku
akidaiwa kujigamba kuwa atafanya jambo lolote baya zaidi dhidi ya mtoto
huyo.
“Baada ya mwanamke huyo kudhaminiwa polisi, alisikika akijigamba kuwa
mtoto huyo atamfanyia jambo lolote lile, kwani hawezi kumwaribia
maisha yake kwa mumewe,” alidai Mshora.
Baadhi ya mashuhuda walidai kusikia kilio kinachotokana na kipigo
kutokana kwa mtoto huyo hata wakati mwingine mwanamke huyo humtoa nje
kutokana na kudai kujisaidia haja kubwa ndani ya nyumba.
“Sisi tuligundua baada ya kila siku kusikia mtoto analia kwa kipigo,
tena alikuwa akichovya fimbo aliyompigia katika kinyesi na kumlisha,”
alidai mmoja wa mashuhuda.
Walisema kuwa kutokana na udogo wa mtoto huyo, anashindwa kufungua
mlango hatua inayomlazimu kuenda haja kubwa ndani ya nyumba.
Wananchi hao walidai kuwa mwanamke huyo ufanya ukatili huo mara kwa
mara, hasa pale mume wake anapokuwa visiwani kwenye shughuli zake za
uvuvi.
Wakati huo huo, mtoto mdogo aliyeozwa kwa mwanaume wa miaka 54,
amepelekwa kwenye kituo cha kulea watoto kiitwacho Jipe Moyo, kilichoko
mjini Musoma, ili aweze kutunzwa huko na kusomeshwa.
Mtoto huyo aliolewa na mwanamume huyo baada ya kutoa kishika uchumba
kiasi cha sh 55,000 kwa baba mzazi wa mtoto huyo, ambapo hivi sasa
wazee hao wapo mahabusu kutokana na kukosa dhamana.
credit, tanzania daima
0 comments:
Post a Comment