pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

DEREVA AMBAKA MWANAFUNZI WA MIAKA 14 HUKO IRINGA

Watu wawili wafariki dunia na mwingine kubakwa katika matukio matatu tofauti mkoani Iringa likiwemo la mkulima wa Kijiji cha Udekwa kukutwa chumbani kwake akiwa amefariki dunia.
 Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 16 machi majira ya saa 3 kamili asubuhi huko maeneo ya Kihesa Ngome.
Kamanda alimtaja marehemu aliyefahamika kwa jina la Dotto Kigoda (18) na kusema chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa.
Tukio lingine mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Fredy Kihwelo (32) mkulima wa Mseke alikutwa juu ya mti akiwa amejinyonga kwa kutumia kanga. 
polisi
Tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 16 machi majira ya saa 5 kamili asubuhi maeneo ya Pipeline wilaya ya Iringa Vijijini huku chanzo cha tukio hilo kikisemekana kuwa marehemu alikuwa na ugonjwa wa akili.
 
Mbali na matukio hayo mawili ya vifo, Kamanda Mungi alisema mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Lemi Chang’a alimbaka binti wa miaka 14 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Lipuli.
 Tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 15 machi majira ya saa 7 kamili mchana huko maeneo ya Kijiji cha Mwika kata ya Ulanda kilichopo wilaya ya Iringa Vijijini.
Kamanda alisema mtuhumiwa alimfanyia kitendo hicho mwanafunzi huyo ndani ya gari la mtuhumiwa na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri mwanafunzi huyo, huku chanzo kikiwa ni tamaa ya mwili hata hivyo mtuhumiwa anatafutwa na jeshi la polisi.

0 comments:

Post a Comment