Bondia
wa ngumi za kulipwa Fadhili awadh amefariki dunia katika hospital ya
mwananyamala baada ya kuugua kwa siku kadhaa. Fadhili awadh alikuwa ni
miongoni mwa mabondia waliochaguliwa kucheza mpambano wa ubingwa tarehe
29 mwezi huu wa tatu dhidi ya mpinzani wake toka tanga Alan Kamote,
hivyo pia alikuwa katika maandalizi ya mpambano huo.
Sababu
ya kifo chake kwa ripoti ya daktari wa mwananyamala kwa kiongozi wa
ngumi Ibrahim Kamwe ni kuwa fadhili alikuwa na malaria na alitumia dozi
ya metakelfin, na hali ilibadirika pale alipojaribu kufanya mazoezi na
kujisikia vibaya na kuwahishwa katika hospitali hiyo ambayo alikaa kwa siku mbili akiendelea na matibabu na hatimae umauti ulipomkuta.
Fadhili awadh mwenye umri wa maika 32 alikuwa anaendelea vizuri katika
mchezo huo kiasi cha kufikia kucheza pambano la ubingwa katika ukumbi wa
PTA sabasaba, akiwasindikiza mabondia japhet kaseba na Thomas mashali .
sisi tulimpenda lakini mungu alimpenda zaidi ,Ailaze roho ya marehemu
Fadhili awadh “tiger” peponi.Mwili wa marehemu umesafilishwa kwenda morogoro kwa ajili ya maziko.
Bondia huyo enzi za uhai wake alicheza mapambano 12 amepoteza 5 na kushinda 7 ambapo mpambano wake wa kwanza katika harakati za ngumi za kulipwa alicheza tarehe
10,09,2010 |
na
Ramadhan Seif, ambapo alishinda kwa TKO ya raundi ya pili
na mpambano wake wa mwisho alicheza na Mfaume Jumanne feb 16 katika ukumbi wa kwa mama rajabu chanika na kufanikiwa kushinda kwa K,O ya raundi ya pili.
crd, gumzo
0 comments:
Post a Comment