Taarifa kutoka Mtwara ambazo
zimethibitishwa na jeshi la Polisi zinaarifu kuhusu Mtumbwi ambao
umezama wakati ukivuka kutoka kitongoji cha Ng’wale kwenda ng’ambo ya
pili ambapo ndiyo sehemu waliyokuwa wanashukia abiria waliokuwepo.
Tayari watu 21 wamefikishwa katika hospital ya mkoa wa Mtwara kwa
matibabu ambao wote ni wakina mama pamoja na mtoto mmoja wa kiume wa
mwaka 1 huku waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo wakiwa ni wakina mama
3.
Mtumbwi huo unahisiwa ulikuwa na abiria 24 ambapo pamoja na
wahusika wawili wa mtumbwi huo kwa pamoja, jumla ya watu waliokua kwenye
mtumbwi ni 26 ambapo Polisi wanasema kina mama hao walikua wanatoka
kutafuta samaki kwa ajili ya biashara.
Jeshi la polisi bado linamtafuta aliekua anauendesha huo Mtumbwi
ambae inasemekana aliogelea na kutoweka baada ya mtumbwi kuzama.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika ingawa baadhi ya abiria
wanadai ni upepo mkali na mvua iliyokuwa inanyesha kwenye eneo hilo.
gumzo
0 comments:
Post a Comment