Oparesheni Nzito ya kuzuia Bodaboda na Bajaji zisifanye safari
zake kutoka Mwenge na maeneo mengine kuelekea mjini Posta imechukua
sura mpya leo baada ya Askari wa Usalama wa Barabarani kuanza kukamata
Bodaboda na Bajaji zote zinazovuka Mwenge kuelekea Posta, Zoezi hilo
ambalo limefanyika Mwenge Mataa Jijini Dar limeendelea kufanyika na
kufanikiwa kuwanasa wengi.
Kwa mujibu wa Msemaji na Muongozaji wa Oparesheni hiyo ambaye
hakutaka kutajwa jina lake alisema kwamba wameamua kufanya hivyo ili
kuzuia Msongamano wa Magari pamoja na bodaboda pia Bajaji kuelekea Mjini
Posta, Aliongeza kuwa kumekuwa na uhalifu sana wa Silaha unaotumiwa na
bodaboda hasa maeneo ya mjini hivyo ndio maana wameamua kuzuia.
“Tumefanya hivi ili kuepusha
msongamano kuelekea Posta, lakini pia kumekuwa na uhalifu sana
unaotumiwa kwa njia ya Bodaboda hivyo tunafanya oparesheni hii ili
kupunguza tatizo hili. Tulicho kifanya tumewaruhusu kufanya safari
pembezoni mwa mji tuu hivyo Eneo la Mwenge kwa sasa Limeingia katika
zone ya eneo la Mjini,Kama tuliweza kuzuia Daladala ndogo”Hiace” pia na
hawa watakuja kuelewa ingawa ni zoezi gumu na linalo hitaji elimu ya
ziada ambayo tumesha anza kuwapa na tunaendelea kuwapa” alimalizia kwa
kusema “Pia hii ni Oparesheni ya kawaida tuu ya kukamata wale ambao
hawana Leseni za kuendesha vyombo hivi pamoja na makosa mbalimbali” alisema Polisi huyo.
Kwa mujibu wa madereva wa Bodaboda na Bajaji wamesema kwamba huo ni
uonevu kuwakataza wao wasiweze kwenda Mjini kwani na wao wanatafuta
ridhiki yao na wameomba Serikali iwasaidie wapatiwe njia mbadala ya wao
kwenda maeneo hayo.
Wanao ruhusiwa kwenda Posta na Bajaji au Bodaboda ni wale ambao ni
wamiliki binafsi na wanatakiwa wapite njia hizo wakiwa Bila abiria
yoyote.
0 comments:
Post a Comment