Mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 35 amekutwa porini akiwa uchi wa mnyama na hawezi kuongea hali iliyozua hofu kwa wananchi na kudai ni msukule.Mwanamke huyo baada ya kupatiwa maji na chakula.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni maeneo ya Pugu Mnadani, wilayani
Ilala jirani kabisa na Pori la Hifadhi ya Kisarawe mkoani Pwani. Baadhi
ya wakazi walimhusisha mwanamke huyo na imani ya msukule wakidai huenda
alitoroka kutoka kwenye makazi yake kabla ya kukatwa ulimi.
Akizungumza na gazeti hili, shuhuda mmoja wa tukio hilo, Said alisema
baada ya kumkuta katika hali hiyo walianza kwa kumsitiri kwa nguo kisha
mwanamke mmoja mganga alimlisha dawa ya kienyeji ndipo akaanza
kuzungumza lakini kwa shida.
Wasamalia wema wakijaribu kumhoji mama huyo.
“Tulimuuliza jina lake akasema anaitwa Tumsifu Yesu. Alidai ameishi
kwenye pori hilo kwa kipindi kirefu bila kujua alifikaje kwa vile kwao
ni Iringa. “Cha kustaajabisha zaidi pale alipopewa chakula alifanikiwa
kula maandazi arobaini na maji lita tano ndani ya dakika kumi tu,”
alisema shuhuda huyo.
Akaendelea: “Baada ya kumaliza kula alionesha ishara ya msalaba kwa
kumshukuru Mungu. Ndipo akapelekwa serikali ya mtaa na baadaye Kituo cha
Polisi cha Pugu kwa msaada zaidi,” kilisema chanzo hicho.
CREDIT: GPL
0 comments:
Post a Comment