Mgombea Ubunge katika Jimbo la
Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ramadhani Mgaya (pichani juu)
kupitia chama cha AFP amejeruhiwa kwa mapanga na watu wasio julikana.
Mgaya amesema amevamiwa na
kujeruhiwa na mtu ambaye hamfahamu majira ya saa sita za usiku akiwa
katika nyumba ya kufikia wageni ya Goodtime Chalinze.
“Nimevamiwa na kujeruhiwa na mtu ambaye simfahamu ahsante uongozi wa Chadema kwa kunisaidia,” alisema Mgaya.
Mgaya amesema ameumia mikononi wakati akipangua nakujitetea maana mvamizi alikuwa na panga.

Mbali na yeye pia amesema
kiongozi wa Chadema, Mwita Waitara naye alijeruhiwa kwa kuwa alikuwa
mmoja ya watu waliokuwa wakimsaidia.
0 comments:
Post a Comment