TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Maadhimisho ya siku ya Mashujaa
(Karume Day) kwa mwaka 2014 yatafanyika siku ya Jumatatu tarehe 7/4/2014 Ofisi
Kuu ya CCM Kisiwandui kuanzia saa 2.30 asubuhi
Shughuli mbali mbali za maadhimisho
hayo zitafanyika ikiwa ni pamoja na kusomwa khitma ya kuwaombea dua wazee wetu
waliotangulia pamoja na kuweka mashada ya mauwa katika kaburi la Marehemu Mzee
Abeid Amani Karume.
Kwa taarifa hii chombo chako cha
habari kinatakiwa kishiriki kikamilifu maadhimisho hayo.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO
ZANZIBAR
0 comments:
Post a Comment