MAUZA
uza matupu kaburi la mtoto Agnes Mlawa (8) mkazi wa Ilala katika
Manispaa ya Iringa aliyezikwa mwaka jana na leo baba wa mtoto huyo
kakuta chungu cha ajabu chenye damu,maini na kichwa cha ndege
kimechimbiwa kaburini.
Tukio
hilo la aina yake limetokea leo majira ya saa 2 asubuhi katika
makaburi ya Makanyagio mjini Iringa wakati baba mzazi wa mtoto huyo
Bw. Mlawa wakati akichembua kaburi hilo na mara baada ya kumaliza
ghafla alishuhudia tukio hilo la chungu cha ajabu kuibuga juu ya
kaburi hilo .
Mzazi wa Marehemu Afunguka
”
mimi hapa leo nilikuja kusembua kaburi la mwanangu ila baada ya
kumaliza ghafla nilikuta kama damu zinaruka juu kutoka kaburini na
baada ya kuchunguza ndipo nilipoona chungu hicho kikiibuka huu ya
kaburi “
Alisema
kuwa chungu hicho kilikuwa kimefungukwa na kitambaa cheusi juu
ambacho kimelowa dawa na kufungwa kamba ya nguo ya kijani na
kutokana na tukio hilo la ajabu alilazimika kuacha jembe juu ya
kaburi na kukimbia kuita watu wanaopita barabarani ili kuomba
msaada zaidi.
Mzazi
huyo anadai kuwa mazingira ya kifo cha mtoto wake yalikuwa ni ya
kushangaza baada ya kuugua kwa muda wa siku nne pekee na kufariki
dunia .
Hata
hivyo alisema kwa kuwa kwa upande wake haamini mambo ya
kishirikiana hakuona sababu ya kumwita mganga wa kienyeji kwa
ajili ya kushughulikia kuchoma chungu hicho na badala yake kuamua
kuifanya kazi hiyo mwenyewe hasa akiamini nguvu ya Mungu zaidi.
”
Napenda kuwashukuru wananchi waliofika hapa kwa kunitia nguvu na
pia kuwashukuru madereva boda boda akiwemo kijana Ahmed kwa
kujitolea mafuta ya Petrol kwa ajili ya kukichoma chungu hiki “
Mbali
ya mzazi huyo kujitolea kuchuma chungu hicho na kuteketeza vitu
vilivyo kuwemo ndani wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo
walilazimika kutimua mbio kuhofu zoezi hilo la uchomaji wa tunguli
hizo
|
0 comments:
Post a Comment