Wapiganaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina
HAMAS wamewajeruhi vibaya makomando 4 wa baharini wa utawala ghasibu wa
Israel. Habari zinasema kuwa, makomandoo hao wenye uzoefu wameshindwa
kuingia kwenye eneo la Sudanyia baada ya kukabiliwa na upinzani kutoka
kwa wanamapambano wa Brigedi ya Qassam ambalo ni tawi la kijeshi la
HAMAS. Wazayuni walikuwa wakijaribu kuanzisha hujuma ya nchi kavu leo
alfajiri wakati mapigano makali yalipotokea kati yao na wanamapambano wa
Kipalestina.
Umoja wa Mataifa umezidi kutoa wito kwa pande mbili za Palestina na
Israel kusitisjha mapigano mara moja. Hadi sasa mashambulizi ya kinyama
ya utawala haramu wa Israel huko Gaza yamesababisha kuuawa shahidi
Wapelstina 155.
Wakati huohuo serikali ya Senegal imelaani mashambulizi ya utawala
haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kuutaka Umoja wa Mataifa
uchukue hatua za haraka kuwasaidia Wapalestina. Taarifa ya serikali ya
Senegal imetaka UN kupeleka misaada ya dharura kwa watu wa eneo la Gaza
sambamba na kuilazimisha Israel ikomeshe mashambulizi yake mara moja.
0 comments:
Post a Comment