Ripota
toka nchini Kenya Julius Kipkoech anaripoti kwamba nchi hiyo inarejea
kwenye headlines kuhusu maswala ya kubuni sheria za kipekee ambapo sasa
bunge la kitaifa linapanga kujadili sheria inayopendekezwa kwamba raia
yeyote wa kigeni anayepatikana akishiriki uhusiano wa jinsia moja
ahukumiwe kupigwa mawe hadharani hadi kufa na kama ni raia wa Kenya basi
ahukumiwe kifungo cha maisha jela.
Mwandishi
na mdhamini wa sheria hiyo Edward Onwong’a Nyakeriga anapendekeza
kuharamishwa kwa ulawiti na kuhukumiwa jela kwa wanaotenda kosa hilo
huku akisisitiza” “Upo umuhimu wa kuwalinda watoto na vijana ambao
wanalengwa na dhulma ambazo kwa mda mrefu zinaepukwa kutokana na
mabadiliko, teknolojia na habari isiyo chujwa na watoto mayatima kukosa
mwakilishi pamoja na majaribio ya wanaoshiriki uhusiano wa jinsia moja
kuwalea watoto ilihali wanaendeleza uhusiano wao”
Mswada
huu wa chama cha Republican Liberty Party unaharamisha uhusiano wowote
wa jinsia moja na tayari spika wa Bunge la kitaifa Kenya Justin Muturi
ameupokea na kuuwasilisha kwa kamati ya sheria bungeni ambayo
inatathmini kisha kutoa ripoti kwa bunge.
Muswada
huo pia unapendekeza kupigwa mawe hadharani hadi kufa kwa mtuhumiwa
anayepatikana na kosa la kuwalawiti watoto wadogo au anayefanya kitendo
hicho na kumuambukiza mtoto virusi vya ukimwi ambapo tayari wabunge 78
wamekubali kuunga mkono muswada huo kuwa sheria na wengine zaidi
wanaendelea kushawishiwa.
Haya
yanajiri wakati Bunge la kitaifa la Kenya likibuni kikundi mseto cha
wabunge kuhusu maisha ya walio katika uhusiano wa jinsia moja na
wameahidi kutoa mwelekeo wa jinsi ya kushughulikia jambo hilo huku
muswada huu ukitarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa wanaotetea haki
za binadamu.
Mwandishi
wa vitabu maarufu nchini Kenya Binyavanga Wainaina amekua miongoni mwa
waliojitokeza hadharani na kukiri kushiriki mapenzi ya jinsia moja na
wakati huohuo Mashirika ya kutetea haki za wanaoshiriki mapenzi ya
jinsia moja hivi karibuni yaliwasilisha pendekezo la kutaka Wabunge
kuondoa sheria zote zinazowazuia kuishi maisha yao kama watu wengine.
Katiba
ya Kenya mwaka 2010 imeharamisha ndoa ya jinsia moja japo haiharamishi
moja kwa moja uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja ambapo pia mwezi
uliopita utafiti uliofanywa na kampuni ya Ipsos Synovate umeonyesha
kwamba 64% ya Wakenya wanaamini kwamba hisia za kushiriki mapenzi na
jinsia sawa ni jambo la kujifunza ilihali 14% kati yao wanaamini watu
hao huzaliwa walivyo.
0 comments:
Post a Comment