
Wanamapambano wa Palestina wameanzisha wimbi jipya la
mashambulizi ya makombora katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni
kujibu mashambulizi ya kikatili yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa
Ghaza. Leo Jumapili wanamapambano wa Palestina wameshambulia vitongoji
mbalimbali vya walowezi wa Kizayuni kama vile Sdot, Negev, Nahal Oz,
Alumim na Eshkol. Ving'ora vya tahadhari vimesikika pia leo katika
vitongoji vya Hof Ashkelon, Eshkol na Sha'ar HaNegev. Wakati huo huo
jeshi la utawala wa Kizayuni limekiri kuwa Harakati ya Mapambano ya
Kiislamu ya Palestina ina nguvu ambazo hazikutarajiwa na Wazayuni.
Televisheni ya Nasim imenukuu duru za Kiarabu zikisema kuwa, jeshi la
utawala wa Kizayuni leo limesema kwamba, wanamapambano wa Palestina
wamefanikiwa kupenya na kuingia katika kitongoji cha walowezi wa
Kizayuni na kambi ya kijeshi ya Zakim ya Israel. Israel umewataka
walowezi wa Kizayuni wakimbilie kwenye mahandaki hadi watakapopewa
taarifa zaidi. Katika upande mwingine Hamas imemlaumu Ban Ki moon,
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa msimamo dhaifu sana aliouchukua
kuhusu jinai za Wazayuni huko Ghaza na kusema kuwa, Ban ni mshirika wa
jinai za Israel. Televisheni ya "Filastin al Yawm" imemnukuu msemaji wa
Hamas, Sami Abu Zuhri akisema hayo leo na kuongeza kuwa, utawala wa
Kizayuni unashambulia hata shule na vituo vya Umoja wa Mataifa huko
Ghaza, lakini Ban Ki moon ameshindwa kuchukua hatua yoyote ya maana.
0 comments:
Post a Comment