KATIBU wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Paul
Makonda amefanya tukio la iabu na fedheha kwake na chama chake la kumfanyia fujo aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba. Makonda akiwa mmoja wa viongozi CCM, aliongoza kundi la vijana wapatao 15 kufanya fujo zilizosababisha mdahalo uliyokuwa aumeandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kujadili Katiba mpya inayopendekezwa, kusitishwa Katika vurugu hizo, Jaji Warioba na viongozi wenzake waliondolewa jukwaani chini ya ulinzi mkali baada ya vijana hao kuwafanyia vitendo vya
udhalilishaji wakitakankuwadhuru.
Pamoja na Makonda kujitete kwamba hakumpiga Jaji Warioba bali alikuwa katika harakati za kumsaidia asishambuliwe, bado tunalaani tukio hilo la aibu kwa taifa huku tukiamini kwamba vyombo vya dola vitamshughulikia na CCM itaomba radhi kwa upuuzi wake. CCM inapaswa kuwajibika aibu hii kwa sababu mbalimbali; mosi, chama hiki ndicho kinaongoza Serikali iliyoko madarakani, hivyo suala la usalama wa wananchi liko mikononi mwake, lakini kwa tukio la juzi vyombo vya dola havikuwepo ukumbini. Hapa kwanini tusiamini lilipangwa.
Pili, Jaji Warioba ni kiongozi mkuu mstaafu wa nchi, ambaye kwa mujibu wa taratibu za usalama wa Taifa bado anapaswa kupewa ulinzi wa kutosha, vile vile kwa tukio la juzi, vyombo vya dola vilikuwa na taarifa ya mdahalo huo, kwanini ulinzi haukuimarishwa.
Tatu, kama chama makini kinachounda serikali iliyoasisi mchakato wa katiba ambao unaelekea ukingoni kwa amani na utulivu kwa pande zinazosigana kubishana kwa hoja, CCM ilikuwa na wajibu wa kuhakikisha haiwi sehemu ya kuanzisha au kufadhili vitendo vya aibu kama vilivyofanywa na kiongozi wake. Kwa sababu hizi, tunaamini kwamba CCM wanapaswa kujitakasa katika aibu hii kwa kumwaomba radhi Jaji Wariobanna wenzake pamoja na
Watanzania kwa ujumla kutokana na upuuzi uliofanywa na kiongozi wao kwa dhamira ovu.
Ikumbukwe kwamba, hii si mara
kwanza kwa Makonda kufanya vitendo vya kuwadhalilisha wazee halafu CCM ikakaa kimya pasipo kumkemea wala kumchukulia hatua. Januari 28, mwaka huu, Makonda kwa mwamvuli wa UVCCM, alifanya mkutano na waandishi wa habari na kumtolea matusi ya nguoni, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa lakini hakuna kiongozi yoyote wa CCM aliyemkemea. Akiwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Makonda katika moja ya michango yake bungeni, aliwatusi wenyeviti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF na James Mbatia wa
NCCR-Mageuzi akiwaita uzao wa shetani, na alipotakiwa na kiongozi wa dini kufuta kauli hiyo alikataa. Sasa kwanini tusiamini hii ndiyo taswira ya CCM ya sasa?
0 comments:
Post a Comment