Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda , Eliakim Maswi, Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi
Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia , Jumanne, Desemba 23,
2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa
Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam
imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha
Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama
ilivyorekebishwa)”ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu
kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu
Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim
C. Maswi utakapokamilika.Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia imekariri
kauli ya Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa jana, Jumatatu,
Desemba 22, 2014 ambako Rais alisema:
“Kuhusu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa
na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka
kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za
kinidhamu zitachukuliwa.”
Ndugu Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Ndugu Frederick Werema pamoja na Mawaziri wawili walituhumiwa wakati wa Kikao cha Bunge kilichopita kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakati
huo huo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine
zinazochukuliwa, Shirika la Umeme (TANESCO) waendelee na majadiliano na
IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha tozo la uwekezaji (capacity charge)
zaidi ya punguzo la awali lililopatikana kupitia Kituo cha Kimataifa cha
Kusuluhisha Migogoro ya Kimataifa
0 comments:
Post a Comment