Kituo cha Ikwiriri,Wilayani Rufiji kilishambuliwa usiku wa kuamkia
leo na watu waliojihami na silaha na kusababisha vifo vya Maaskari
wawili na wengine wakijeruhiwa vibaya kufuatia tukio hilo.
Habari kutoka Wilayani Rufiji mkoa wa Pwani nchini Tanzania
zinaarifu kuwa watu waliokuwa na silaha wamefanya shambulio kubwa usiku
wa kuamkia leo na kusababisha hasara kwa Maaskari waliokuwa zamu kwenye
kituo hicho.
Hata
hivyo washambuliaji walichukua silaha mbalimbili zilizohifadhiwa katika
kituo hicho,wakaazi wanasema walisiki milio ya risasi zikirindima hovyo
na kuwasababishia khofu.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Pwani Urich Matei amethibitisha kutokea shambulio
hilo na kusema kuwa shambulio hilo limetokea saa 8:00 usiku na
kusababisha vifo vya Maaskari Polisi wawili na silaha kadhaa kuchukuliwa
ambazo zilihifadhiwa kwenye kituo hicho.
Ni
shambulio la kwanza kufanyika nchini Tanzania tangu kwanza kwa mwaka
huu 2015,Mashambulio mengine kama haya pia yalifanyika kwenye vituo vya
Polisi Kimanzichana,Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani,na Wilaya ya Bukombe
mkoani Geita nchini Tanzania.
Serikali
kibaraka nchini Tanzania inawashikilia mamia ya Waislaam na kuendelea
kuwapa adhabu yalio na kinyume na haki za kibinaadam kwa kisingizio cha
tuhumu za Ugaidi na wengine ikiwaua ambapo tukio la mwisho kikosi cha
kupambana na Ugaidi nchini humo iliwaua vijana kadhaa katika miji ya Arusha,Morogoro na Zanzibaar.
0 comments:
Post a Comment